juzi basi, nyanya wa mama yangu alipatwa na jeraha kutokana na kuanguka toka juu kitandani mpaka sakafuni. akapelekwa hospitalini ili kuchunguzwa na kupata tiba. sote tukawa tunampitia kumjulia hali na ilipokuwa desturi yake, tukacheka na kutaniana kwenye wodi utadhani hakuwa mgonjwa!
nilipotoka huko, nilifikiria sana. fikira zenyewe ziligonga kuwa yeye ndiye shina la familia yetu na alivyotoka mbali, hatuna budi kumshukuru Mola kumfikisha mpaka alipo. Isitoshe, wengu wetu hatukupata fursa ya kuwaona wazee wa wazazi wetu, hivi mimi najihesabu kubarikiwa sana kumwona nyanya wa mama! isitoshe tena, tukaweza kukaa chini na kuwa na mazungumzo ya maana, akinipa ujasiri na ufahamu wa mambo.
kisha nikawaza sisi tulivyo na watoto wetu wanavyolelewa. Kama huku si shida, basi sijui nilitamkie neno gani. Watoto waliolelewa na runinga na "mobiles". Wasiojua tofauti katika umri na heshima. Naweza kuendelea lakini sote katika jamii tunajionea.
Nikafikia kuwaza, yaani sisi katika shida na balaa zote hizi tutaweza kukaribia au hata kufikia vyegezo waliofika wazazi wetu. Au babu zetu?